LAAC kusimamia kikamilifu rasilimali za umma

0
476

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imesema itahakikisha rasilimali za umma zinazopelekwa kwenye halmashauri zinatumika kama ilivyokusudiwa.

Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Selemani Zedi ambaye pia ni Mbunge wa Bukene (CCM), amesema kuwa baada ya kuteuliwa juzi na Spika wajumbe wa kamati hiyo wameanza kupatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo ili waweze kusimamia matumizi ya rasilimali za umma zinazopelekwa kwenye halmashauri zote nchini.

“Kwa mujibu wa majukumu yetu kikanuni tutahakikisha rasilimali za umma zinazopelekwa halmashauri zinatumika kama zilivyokusudiwa na matumizi yote yanafanyika kwa mujibu wa sheria ya fedha ya Serikali za Mitaa,” amesema Zedi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here