MWANAMITINDO, Kylie Jenner na msanii wa miondoko ya hip hop, Travis Scott, juzi jioni walifanikiwa kupata mtoto wa kike.
Taarifa ya Kylie kupitia ukurasa wake wa Twitter, alijifungua salama mtoto mrembo mwenye afya.
Kylie alijifungua katika Hospitali ya Cedars-Sinai iliyopo Jiji la Los Angers ambayo ilitumika na dada zake wawili, Kim na Kourtney, wakati wa kujifungua watoto wao.
Mtandao wa TMZ Septemba mwaka jana uliwahi kuelezea hali ya Kylie, wakati akiwa mjamzito lakini mwanamitindo huyo alikana kuwa na ujauzito huo.