Na AVELINE KITOMARY-DAR ES SALAAM
KAIMU Mkurugenzi wa Dawa na Vifaa Tiba wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba(TMDA), Akida Khea amesema yapo madhara makubwa kiafya endapo mtu atatumia kondomu ambazo hazijathibishwa usalama na ubora wake.
Akizungumza na wakati wa mahojiano maalumu MTANZANIA, Dar es Salaam jana, Khae alithibitisha madhara yanayotokana na matumizi ya kondom zisizo na ubora ni kuambukizwa virusi vya Ukimwi pamoja na magonjwa ya zinaa.
Kutokana na hilo, Khea alisema ni bora watumiaji kuhakikisha ubora wa kondom wanazozitumia ili kuepusha madhara hayo.
“TMDA kwa sasa imebki na jukumu la kulinda afya ya jamii kwa kudhibiti ubora,usalama na ufanisi wa dawa ,vifaa tiba na vitendanishi,bidhaa kama kondomu isipokubalika tunasema haina ubora kwa matumizi nchini.
“Kama kondomu ikithibitishwa haina ubora,ikitumika haiweza kumlinda mtumiaji kwa magonjwa ya kujamiana na Ukimwi… kondomu kama hizi ni hatari kwa afya.
“Huwa tukigundua hazina ubora tunaziondoa haraka kwenye soko, ni vizuri jamii wakatumia zilizothibitishwa, pia ni vizuri wakatoa taarifa endapo watakutana na kondomu zisizo na ubora,”alieleza Khea.
Alitoa wito kwa jamii kuaangali mwisho wa matumizi ya bidhaa (expire date), hasa kwa bidhaa kama kondomu ili kulinda afya zao wenyewe.
“Kama una bidhaa ambazo huna uhakikia nazo ni vizuri ukatoa taarifa TMDA ili tukafanyie uchunguzi na tubaini usalama na ubora wake,”alisshauri Khea.
Katika mwaka wa fedha 2019/20, TMDA ilifakiwa kuondoa sokoni pakiti 17,076, baada ya kushindwa kukidhi vigezo vinavyotakiwa.
Kondomu hizo zilizoondolewa sokoni ni aina tano ambazo ni Life Guard, Ulitimate, Maximum Classic,Prudence naa Chishango.