32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Kusitishwa Tamasha la Fiesta linavyoleta hasara

Elizabeth Joachim

Kisitishwa kwa Tamasha la Tigo Fiesta Jijini Dar es Salaam lililopangwa kufanyika leo Novemba 24 katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam limeleta hasara kubwa kwa wananchi kutoka kona mbalimbali za nchi.

Tamasha hilo la kila mwaka kwa mwaka huu 2018 lilioangwa kufanyika leo lakini limesitishwa kwa sababu zilizopo nje ya uwezo wa waandaaji wake.

Licha ya waandaaji wake kupata hasara kubwa kutokana na kupoteza gharama kubwa za maandalizi ya tamasha hilo pia limeingiza hasara wafanyabiashara mbalimbali na mashabiki wake kwa ujumla.

Wafanyabiashara wa nyama choma, maji, vyakula, soda, bia na vitu vingine mbalimbali, wameingia hasara ya moja kwa moja kutokana na kufanya maandalizi ya kununua idadi kubwa ya bidhaa zao wakidhani wangeziuza kwa wingi leo lakini imekuwa tofauti.

Kutokana na kusitishwa huko itawabidi wafanyabisahara hao wauze bidhaa zao hizo kwa bei ya hasara ama wawekeze kwa muda mrefu hadi wayakapomaliza kuuza bidhaa zao amapo itawalazimu wapate kwa kuziifadhi, kuzilinda na soko la kuuzia bidhaa hizo.

Pia biashara ya usafiri itaingia hasara kwani kama tamasha hilo lingefanyika leo wafanyabioashara ya usafiri ingekuwa neema kwao lakini kusitishwa haitawaletea faida zaidi ya hasara kwa kiasi kikubwa.

Mmoja wa wafanyabiashara wa maji kutoka Temeke, Pendo John akizungumza na Mtanzania Digital amesema kusitishwa kwa tamasha hilo kumesababishia hasara kubwa ya upotevu wa muda na gharama ya sehemu soko la kuuzia kiasi kikubwa cha maji aliyoandaa kwa ajili ya tamasha hilo kabla ya kusitishwa kwake.

“Kiukweli nimepokea vibaya taarifa hizi za kusitishwa kwa tigo fiesta kwa sababu tumechelewa kupata taarifa nilijua kwamba idadi kuwa ya maji niliyonunua ningeyauza kwa wingi leo usiku kwenye tamasha hilo, sasa sijui nayapeleka wapi,” amesema Pendo.

Naye Methood Daniel ambaye ni shabiki amesema taarifa za kusitishwa kwa tamasha hilo kumempa hasara kubwa kwa kuwa aliwalipia nauli marafiki zake wengi kutoka mkoani Mbeya kwa ajili ya Tamasha hilo lakini halitofanyika hivyo ameingia hasara kubwa.

“Binafsi sina cha kuongea zaidi ila nawaza pesa aambazo nimewalipia nauli marafiki zangu wanaoishi Mbeya ili waje Dar kuangalia tamasha hilo, hakuna namna tusubirie labda watajipange siku nyigine,’’ ameeleza Daniel.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles