25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

KUONDOKA KWA NEYMAR, PIQUE AOMBA RADHI

BARCELONA, HISPANIA

BEKI wa kati wa klabu ya Barcelona, Gerard Pique, aliwahi kuwaambia mashabiki wa klabu hiyo kuwa mshambuliaji wao, Neymar hawezi kuondoka, lakini siku chache baadaye akajiunga na PSG, hivyo Pique amewaomba radhi mashabiki kwa kauli hiyo.

Pique amedai kwamba alikuwa anajua kama mchezaji huyo lazima ondoke, lakini aliamua kutumia akaunti yake ya Twitter na kujaribu kuwatuliza mashabiki wa timu hiyo kuwa mchezaji wao bado ataendelea kuwepo kikosini.

“Najua kila kitu kwa sasa kimekaa sawa, naweza kuelezea kwamba nilikuwa najua kuwa Neymar anataka kuondoka ndani ya kikosi chetu, siku ambayo Lionel Messi alikuwa anaoa alituambia kama anataka kuondoka.

“Niliamua kuposti picha kwenye Twitter nikiwa na Neymar na kusema haondoki lakini nilikuwa najua kuwa anataka kuondoka kwa asilimia 100, nilikuwa najaribu kuwatuliza mashabiki huku ikiwa ni posti yangu ya mwisho juu ya Neymar.

“Najua wapo ambao waliamini maneno yangu, hivyo naomba wanisamehe, klabu sasa ipo katika kipindi kigumu kwa kuwa itaendelea kumkumbuka mchezaji huyo kwa yale mazuri aliyoyafanya, alikuwa na mchango mkubwa,” alisema Pique.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles