23.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA UTOAJI VIFAA VYA MAUNGANISHO YA HUDUMA ZA MAJI

Je, wewe ni mkazi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ambaye umeomba huduma ya maji na kukamilisha taratibu zote?

Habari njema ni kuwa, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawataarifu Wananchi wa maeneo yake ya kihuduma katika Mikoa wa Dar es Salaam na Pwani kuwa imeanza zoezi la utoaji wa vifaa kwa ajili ya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi.

Pia Mamlaka inasisitiza Wananchi waliokwisha lipia huduma ya maunganisho mapya kuwasiliana na ofisi ya DAWASA Mkoa wa kihuduma kupata utaratibu wa maunganisho.

Baada ya kukamilisha zoezi la kuwaunganisha wateja wote waliolipia, DAWASA itaendelea kutoa control number kwa wateja wote wanaohitaji huduma.

Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (Bure) na
0735 202 121 (WhatsApp tu)

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles