29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Kubenea kupeleka hoja binafsi bungeni kumuenzi Mengi

Asha Bani, Dar es Salaam

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea anatarajia kupeleka hoja binafsi bungeni kuiomba serikali kuchukua hatua za haraka kuridhia Itifaki ya Mkataba wa Afrika wa haki za binadamu kuhusu haki za watu wenye Ualbino Afrika.

Amesema mkataba huo ulipitishwa katika mkutano wa 30 wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika mwaka jana hivyo anaiomba serikali kufanya marekebisho ya sera ya watu wenye ualbino iliyotungwa 2004 ili kuwasaidia kukomesha vitendo vya kikatili dhidi yao.

Kubenea amesema hayo leo Jumapili Agosti 11, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa ameamua kuwatetea watu hao kutokana na kulipa deni aliloachiwa na Mwenyekiti wa Kampuni Tanzu za IPP, marehemu Regnald Mengi.

“Nimeamua kufanya hivi kutokana na kutaka kulipa deni ambalo nimeachiwa na marehemu Mengi, mimi hili ndiyo deni langu kuenzi alichokuwa anakifanya na si vinginevyo,” amesema Kubenea.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Jimbo la Ubungo, Mussa Geuza amesema anawaomba wabunge wengine kumuunga mkono Kubenea kwani hoja yake ina mashiko na ustawi kwao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles