27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

KUBENEA KUTOA MIL 14 KUMALIZA KERO YA KIVUKO MABIBO

MBUNGE wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea

Na Asha Bani -

MBUNGE wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea ameahidi kutoa Sh. 14 milioni kwa ajili ya ujenzi wa Madaraja mawili  katika eneo la Mabibo Sahara kufuatia kivuko kilichokuwepo kwenye eneo hilo kusombwa na maji.

Kubenea ametoa ahadi hiyo leo alipotembelea eneo hilo  ambapo wananchi wamemueleza adha wanayoipata kutokana na kukosekana kwa kivuko cha uhakika ambapo tangu kivuko cha kawaida kusumbwa na mafuriko, kwa sasa kikundi cha vijana kimejenga daraja kwa magogo ambapo wananchi wanalipia Sh 200  kuvuka.

Aidha katika hatua ya awali Mbunge huyo ametoa kiasi cha sh 150,000/- ili vijana hao wawaruhusu wananchi kupita bure.

Bada ya ahadi hiyo, kulitolea mvutano wa wanachi ambao walikuwa wakivutana juu ya eneo la kujengwa kwa madaraja hayo ya kivuko, lakini Mbunge huyu wa Ubungo alitatua tatizo hilo kwa kuwaeleza wananchi kwamba, wataalamu kutoka manispaa watafika kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu ili kujua eneo sahihi la kujenga daraja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles