Na Asha Bani -
MBUNGE wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea ameahidi kutoa Sh. 14 milioni kwa ajili ya ujenzi wa Madaraja mawili katika eneo la Mabibo Sahara kufuatia kivuko kilichokuwepo kwenye eneo hilo kusombwa na maji.
Kubenea ametoa ahadi hiyo leo alipotembelea eneo hilo ambapo wananchi wamemueleza adha wanayoipata kutokana na kukosekana kwa kivuko cha uhakika ambapo tangu kivuko cha kawaida kusumbwa na mafuriko, kwa sasa kikundi cha vijana kimejenga daraja kwa magogo ambapo wananchi wanalipia Sh 200 kuvuka.
Aidha katika hatua ya awali Mbunge huyo ametoa kiasi cha sh 150,000/- ili vijana hao wawaruhusu wananchi kupita bure.
Bada ya ahadi hiyo, kulitolea mvutano wa wanachi ambao walikuwa wakivutana juu ya eneo la kujengwa kwa madaraja hayo ya kivuko, lakini Mbunge huyu wa Ubungo alitatua tatizo hilo kwa kuwaeleza wananchi kwamba, wataalamu kutoka manispaa watafika kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu ili kujua eneo sahihi la kujenga daraja.