29.3 C
Dar es Salaam
Monday, December 30, 2024

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Kortini kwa kubaka mtoto

AVELINE KITOMARY – DAR ES SALAAM

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, jijini Dar es Salaam, imempandisha kizimbani Selemani Hoza (34)Mkazi wa Kimara Mavurunza kwa shtaka la kumbaka mtoto wa miaka 11.

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Boniface Lihamwike, Mwendesha mashtaka wa Jamhuri Veronika Mtafia mwishoni mwa wiki, alidai kati ya Mei 17 na 18,mwaka jana eneo la Kimara Korogwe, Wilaya ya Ubungo alimbaka mtoto huyo (jina limehifadhiwa), huku akijua ni kinyume cha sheria.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo huku upande wa Jamuhuri ulisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa tena.

Hakimu Lihamwike alisema dhamana yake ipo wazi kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaotoa bondi ya Sh millioni 1 kwa kila mdhamini mmoja.

Mshtakiwa alirudishwa rumande kutoka na kushindwa kukidhi masharti ya dhamana mpaka shauri hilo litakaposomwa tena Mei 13 mwaka huu.

Wakati huo huo, mahakama imempandisha kizimbani Elias John (18) Mkazi wa Kimara kwa shtaka la ubakaji.

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu  Anifa Mwingira,Wakili wa Serikali Matarasa Hamisi alidai kati ya Oktoba Mwaka jana na Februari 26 mwaka huu eneo la Kimara,Wilaya ya Ubungo alimbaka mtoto wa miaka 9 (jina tunalo).

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo huku upande wa Jamuhuri ulisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa tena.

Hakimu Mwingira, alisema dhamana iko wazi kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaotambulika kisheria watakaotoa bondi ya Sh millioni 1.

Hata hivyo Mshtakiwa alishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kurudishwa rumande mpaka kesi yake itakaposomwa tena Mei 13 mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles