22.5 C
Dar es Salaam
Friday, June 21, 2024

Contact us: [email protected]

Korea Kaskazini yahoji upendeleo wa UN

PYONGYANG, KOREA KASKAZINI

SERIKALI ya Korea Kaskazini imekosoa mwenendo usioridhisha na kutia shaka wa Umoja wa Mataifa kutokana na kile ilichokiita kuzipendelea nchi zenye nguvu na kusisitiza kuwa nchi yao itasimama kidete kukabiliana na vikwazo dhidi yake.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini imetangaza kwamba, jumuiya za kimataifa, ukiwamo Umoja wa Mataifa zinapitisha maazimio ambayo yanadhamini masilahi ya nchi zenye nguvu duniani.

Vilevile imewakosoa viongozi wa UN kutokana na hatua yao ya kuziwekea vikwazo nchi wahanga ambazo zimesimama imara dhidi ya watenda jinai, imesema kuwa vikwazo hivyo vinakiuka waziwazi haki ya kujitawala nchi za dunia na kwamba Korea Kaskazini imeazimia moja kwa moja kukabiliana na mienendo hiyo.

Taarifa ya wizara hiyo pia imesisitizia uwezo wa kiulinzi kuwa wenye kuaminika zaidi kwa ajili ya kupatikana uadilifu wa kimataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles