25.8 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Korea Kaskazini kurusha tena bomu la nyuklia

2af6d777-98e6-46ef-b59e-f9f59910e577_cx0_cy5_cw0_mw1024_mh1024_s

SEOUL, KOREA KUSINI

MAOFISA wa Korea Kusini wametahadharisha kwamba huenda Korea Kaskazini ikafanya jaribio lingine la bomu la nyuklia wakati wowote.

Wasiwasi huo unakuja baada ya Ijumaa iliyopita Korea Kaskazini kufanya jaribio linalohesabiwa kubwa zaidi katika historia ya taifa hilo.

Msemaji wa jeshi la Korea Kusini amesema bado kuna shimo la kulipua bomu ambalo halijatumiwa katika eneo la kufanyia majaribio la Punggye-ri, ambalo linaweza kutumiwa kulipua bomu la sita wakati wowote.

Korea Kaskazini ilishutumiwa vikali na jamii ya kimataifa baada ya jaribio hilo la Ijumaa kuongeza hali ya wasiwasi na uhasama.

Jumapili, mmoja wa maofisa wa jeshi la Korea Kusini alinukuliwa na Shirika la Habari la Korea, Yonhap akisema nchi yake ina mpango wa kuuangamiza kabisa Pyongyang, mji mkuu wa Korea Kaskazini, iwapo kutaonekana dalili kwamba nchi hiyo inajiandaa kutekeleza shambulio la kinyuklia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles