25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, August 14, 2022

Kampuni ya kufadhili miradi Afrika yaundwa

image

NAIROBI, KENYA

CHINA na Benki ya Dunia zimeunda kampuni ya miundombinu ikiwa na uwekezaji wa awali wa dola milioni 500 kwa ajili ya kufadhili miradi barani Afrika.

Kampuni hiyo ya Uwekezaji na Maendeleo ya Miundombinu Ng’ambo ya China (COIDIC) itawekeza na kuendesha miradi kuanzia wazo la mradi hadi upembuzi yakinifu.

Pia itafuatilia matumizi ya fedha na kushiriki katika shughuli za kibiashara.

Wanahisa wa kampuni hiyo ni pamoja na Benki ya Maendeleo China (CDB), Mfuko wa Maendeleo China-Africa (CADFund) na Kampuni ya Uwekezaji Ng’ambo ya China Gezhouba.

Wengine ni Kampuni ya Kimataifa ya Mawasiliano na Utafiti, Mipango na Ubunifu (CISPDR), Shirika la Uhandisi la China na Kampuni ya Uwekezaji wa Nishati.

Naibu Mkurugenzi wake, Nicholas Mitsos, alisema wanataka kuonesha kuwa Wachina na taasisi nyingine zilizopo katika mataifa ya magharibi zinaweza kuungana na kujenga miundombinu ya umma katika mataifa yanayoendelea.

Kampuni hiyo ya pamoja ya uwekezaji imelenga kuasili mkakati wa kugharimia miradi kama wa Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu Asia (AIIB) na Benki ya Maendeleo Mapya (NDB) ambayo pia inajulikana kama Benki ya BRICS, ambayo ina mataifa karibu 60 kama wanahisa.

COIDIC imepanga kuendesha miradi mikubwa ya miundombinu kwa kushirikiana na Afrika na wadau wengine wa maendeleo, wakopeshaji, viongozi, wahandisi na mameneja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,695FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles