27.9 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

KOCHA MPYA SIMBA ADUWAZWA BUNJU

NA THERESI GASPER -DAR ES SALAAM

KOCHA mpya wa Simba, Sven Vanderbroeck, ametinga kwa mara ya kwanza katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika jana kwenye Uwanja wa Bunju (MO Simba Arena), Dar es Salaam na kupokelewa kwa shangwe na mashabiki wa timu hiyo.

Vanderbroeck aliingia mkataba wa mwaka mmoja wa kuinoa timu hiyo juzi akirithi mikoba ya Patrick Aussems aliyetimuliwa mwezi uliopita.

Kocha huyo raia wa Ubelgiji, aliwasili uwanjani hapo saa 9:45 akiwa katika gari namba T 927 DQB, aina ya Wsth akiwa ameongozana na kocha wa viungo,  Adel Zrane.

Baada ya kufika uwanjani hapo, alitumia dakika tano ndani ya gari kabla ya kushuka na kwenda moja kwa moja katika vyumba vya kubadilishi nguo wachezaji, akiongozwa na Meneja wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu.

Baada ya kushuka katika gari, alishangazwa na mashabiki wengi waliojitokeza uwanjani hapo ambao walianza kumshangilia kwa kumpigia makofi na miluzi.

Baada ya dakika tano kupita akiwa katika vyumba vya kubadilishia nguo, alitoka na kukaa katika kiti na kuangalia mazoezi yaliyokuwa yakisimamiwa na kocha msaidizi, Seleman Matola, huku akiwa makini kufuatilia kila hatua na kuandika baadhi ya vitu katika kijitabu chake (notebook) kulingana na kile alichokiona.

Katika mazoezi hayo, Zrane aliwakimbiza wachezaji kwa kuzunguka uwanja mara sita kwa lengo la kutafuta pumzi kabla ya kufanya mazoezi ya viungo huku Vanderbroeck akifuatilia hatua kwa hatua.

Baada ya mazoezi ya hayo kukamilika, Matola aliwagawa wachezaji katika makundi na kuanza kupiga pasi fupi fupi, kabla ya kuunda vikosi viwili na kucheza mechi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles