26.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Kocha Kenya afurahia kuwepo Misri

CAIRO, MISRI

KOCHA wa timu ya taifa Kenya, Sebastien Migne, amesema furaha yake ni kuiona timu hiyo ikiwa nchini Misri kwenye michuano mikubwa barani Afrika na angejisikia vibaya endapo wangekuwa nyumbani na kuangalia kwenye runinga.

Hata hivyo, kocha huyo amewataka mashabiki wa taifa hilo kujivunia nafasi hiyo ya kushiriki Afcon bila ya kujali kitakacho tokea.

Huu ni mwaka wa kwanza kwa Kenya kushiriki michuano hiyo baada ya miaka 15, wamepangwa kundi C wakiwa pamoja na Algeria, Senegal na majirani zao Tanzania.

Hii ni mara ya sita kwa Kenya kushiriki michuano hiyo, huku mara tano zilizopita hawakuwahi kufanikiwa kupita hatua ya makundi, wakishinda mchezo mmoja kati ya jumla ya michezo 14 tangu mwaka 1972, wamepoteza michezo tisa na kutoa sare michezo minne.

“Ni jambo la kujivunia kushiriki kwenye michuano hii kwa kuwa tulikosa nafasi hiyo kwa miaka 15 huku tukiwa nyumbani kuangalia kwenye runinga.

“Naweza kusema kila raia wa Kenya anatakiwa kujivunia, tutahakikisha tunapambana kwa ajili ya kujifunza,” alisema kocha huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles