24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kizimbani kwa kubaka, kulawiti mtoto wa miaka tisa

ERICK MUGISHA (DSJ) na AVELINE KITOMARY – DAR ES SALAAM

MKAZI  wa Kimara Korongwe Jumanne Kunambi (27) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, akikabiliwa na mashitaka ya kubaka na kulawiti mtoto wa miaka tisa.

Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Joyce Moshi, Mwendesha Mashitaka wa Jamuhuri, Ester Chale, alidai kati ya Septemba 2018 hadi Mei 2019 maeneo ya Kimara Korongwe Wilaya ya Ubungo Dar es salaam, mtuhumiwa alimbaka mtoto mwenye umri wa miaka 9.

Katika shtaka la pili mnamo Septemba 2018 hadi Mei 2019 eneo la Kimara Korongwe, mshtakiwa alimuingilia kinyume na maumbile mtoto wa miaka 9.

Mshitakiwa alikana kutenda mashtaka yote mawili mbele ya mahakama na mwendesha mashtaka wa Jamuhuri  alisema “upelelezi wa shauri hili bado unaendelea tunaomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Hakimu Moshi alisema dhamana ipo wazi kwa mshitakiwa kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu wanaofanyakazi kutoka kwenye ofisi zinazotambilika kisheria na wawe na vitambulisho na kusaini bondi ya Sh millioni 1.

Mshitakiwa alirudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza mashariti ya dhamana na kesi itakuja kusomwa tena Juni 17 mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles