Na WAANDISHI WETU
KITENDO cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuacha kususia uchaguzi mdogo, na juzi kutangaza kusimamisha wagombea wa ubunge katika majimbo ya Kinondoni, Dar es Salaam na Siha mkoani Kilimanjaro ni kama kimebadilisha upepo wa kisiasa tofauti na mwanzo.
Ukiacha Siha ambako Chadema imemsimamisha Elvis Mosi, Jimbo la Kinondoni ambalo liko katika Jiji la Dar es Salaam lenye historia ya siasa za upinzani kwa miaka mingi, ndilo linalotazamwa zaidi na watu mbalimbali katika uchaguzi huu utakaofanyika Februari 17.
Hatua ya Chadema kumsimamisha Naibu Katibu Mkuu upande wa Zanzibar, Salum Mwalimu kuwania jimbo hilo, dhidi ya Maulid Mtulia aliyesimamishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kumeelezwa na wachambuzi wa masuala ya kisiasa kuwa ni mapema kutabiri au mtu yeyote kujitapa mshindi.
Mtulia ambaye alijiondoa katika nafasi hiyo anayoiwania tena mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuhama Chama cha Wananchi (CUF), na kujiunga CCM kwa kile alichoeleza kuwa anaunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na Rais Dk. John Magufuli, tayari amekwishasema atarudi kwa kishindo katika jimbo hilo.
HISTORIA YA SIASA ZA DEMOKRASIA DAR
Wafuatialiaji wa masuala ya kisiasa waliozungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, wanasema lolote linaweza kutokea katika uchaguzi huo.
Sababu kubwa zinazotajwa na wachambuzi hao kusimamia kauli yao hiyo ni, historia ya siasa za demokrasia, hasa katika ………….
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya MTANZANIA.