29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

KITUO CHA SHERIA CHAITAKA BUNGE KUCHUNGUZA ‘WASIOJULIKANA’

WADAU na mashirika ya utetezi wa Haki za Bindamu wametoa mapendekezo 11 ikiwemo kuhakikisha inaharakisha uchunguzi na kuwanasa ‘watu wasiojulikana’ waliojaribu kumuua Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Seria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo-Bisimba amesema, watetezi wa haki za binadamu wamechoshwa na vitendo vya kinyama na kikatili vinavyotishia amani nchini ambapo ametaka kuundwa kwa tume huru itakayoongozwa na Bunge ili kufanyika uchunguzi wa haraka wa muda mfupi watuhumiwa wachukuliwe hatua.

“Iwapo Serikali itashindwa kuwasaka watu hawa na kuwatia mbaroni ni vyema itafute msaada kutoka nchi nyingine zenye mbinu zaidi na sasa ifike wakati serikali ikaona haja ya kuhakikisha inawasaka watu waliotajwa au kumshambulia aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Sanaa, Nape Nnauye na waliovamia kituo cha Radio cha Clouds FM.

“Tunaomba waliovamia pia mkutano wa CUF maarufu kama wasiojulikana wakamatwe na kufikishwa mahakama haraka iwezekanavyo ili kujibu tuhuma zinazowakabili,” amesema.

Wakati huohuo, kituo hicho kimemuomba Rais John Magufuli kutumia wadhifa wake kubadili vifungu vya sheria inayoelekeza adhabu ya kifo ambayo amesema walikuwa wakipinga kwa muda mrefu adhabu hiyo kwa sababu ilikuwa inaenda kinyume na haki za binadamu hivyo wamempongeza Rais Magufuli kwa kuliona hilo na kuanza kulikemea hadharani.

“Tunampongeza rais Magufuli kwa kupinga adhabu ya kifo kwani haina faida yoyote wala haijachangia kupunguza matukio ya mauaji …hivyo wito wetu Serikali ianze mchakato na kubadili sheria hii,” amesema.

 

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles