28 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

Kishimba aitaka serikali iruhusu matumizi ya bangi nchini

RAMADHAN HASSAN,DODOMA

MBUNGE wa Kahama Mjini,Jumanne Kishimba (CCM) ameishauri Serikali iruhusu matumizi ya bangi kwani dawa nyingi za maumivu zinatumia mmea huo.

Kauli hiyo ameitoa leo Mei 20 Bungeni wakati akichangia mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, kwa mwaka wa fedha 2018-2019.

Kishimba amesema dawa nyingi za maumivu zinatokana na bangi hivyo akaitaka Wizara ya Kilimo iwaruhusu wakulima ili walime.

“Sisi wenyewe tunayo bangi ukweli bangi hiyo sio kwa ajili ya kuvuta ni inaenda ,Lethoto na Zimbabwe wameruhusu.

“Gunia moja la bangi ni milioni 4 mpaka 5 bangi yote hii ya Tanzania inaenda katika madawa ya binadamu kuna ubaya gani Serikali itoe vibali ili watu walime bangi .Waziri wa Kilimo awasiliane na wa Afya kwani bangi hailiwi na wadudu ekari moja ya bangi unapata gunia sita,amesema Kishimba.

Akichombeza Spika Ndugai aliwataka Wabunge kuchangia kama ambavyo amechangia Mbunge huyo kwa kujikita katika eneo moja

“Niwape siri muongee kama Kishimba unakuja na kitu chako fulani.unajikita sehemu moja.Hii hoja ni nziti sana Naamini Jenista (Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge,Ajira,Kazi,na watu wenye ulemavu) ameipigia mstari,”amesema Spika Ndugai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles