27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 12, 2024

Contact us: [email protected]

Kipindupindu Dar ‘songombingo’

said meck dsdickNa Veronica Romwald, Dar es Salaam

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesisitiza kuwa taarifa iliyoitoa mwanzoni mwa wiki hii ya kurejea   kipindupindu  Dar es Salaam ni sahihi.

Kauli hiyo ya wizara imetolewa siku chache baada ya Mganga Mkuu wa Temeke kukana kuwapo wagonjwa waliolazwa kwenye kambi maalumu ya wagonjwa wa kipindupindu katika wilaya hiyo.

Vilevile,  juzi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick alisema watendaji wa wizara walipotosha   kuwa ugonjwa huo umerejea jijini humo. Alisema kipindupindu hakipo Dar es Salaam.

Jana  Ofisa Uhusiano wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Wizara hiyo, Catherine Sungura alisema ni kweli ugonjwa huo upo katika jiji hilo.

“Taarifa iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Temeke, akidai  hakukuwa na wagonjwa kipindupindu si sahihi, ukweli ni kwamba ugonjwa huo umerejea  Dar es Salaam,” alisema

Alisema hiyo ni kwa sababu wizara inayo miongozo inayosimamia ufuatiliaji wa magonjwa ya milipuko na miongozo hiyo hutolewa na kusambazwa katika mikoa na wilaya zote nchini.

Sungura alisema katika mwongozo huo taarifa za magonjwa ya milipuko kama kipindupindu  yanapotokea hutolewa taarifa mara moja kwa kutumia ainisho sanifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles