28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Kipa Tottenham aomba radhi mashabiki

LIVERPOOL, ENGLAND

KIPA wa timu ya Tottenham, Hugo Lloris, amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo baada ya kusababisha bao katika dakika za lala salama kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Liverpool juzi.

Katika mchezo huo, Liverpool ambao walikuwa nyumbani walifanikiwa kuutumia vizuri uwanja huo wa nyumbani na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kuwafanya wazidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi.

Hadi dakika ya 90, mchezo huo ulikuwa 1-1, lakini mlinda mlango huyo alijikuta akiwakasirisha mashabiki wake baada ya kushindwa kudaka mpira wa kichwa uliopigwa na mshambuliaji wa Liverpool, Mohammed Salah na kisha kipa huyo kuudaka na kuuangushia miguuni mwa mchezaji wake, Toby Alderweireld ambaye ulimgonga na kuzama moja kwa moja wavuni.

Mlinda mlango huyo alikuwa na nafasi ya kuudaka mpira huo, lakini alijikuta akifanya kosa ambalo liliigharimu timu katika dakika hiyo ya 90.

Hata hivyo, baada ya kufanya kosa hilo, mlinda mlango huyo ameweka wazi kuwa, kosa hilo ni sehemu ya makosa ya mlinda mlango.

“Siwezi kujua kwanini tukio kama hilo liliweza kutokea, nilijaribu kuukamata mpira huo mara mbili lakini nilishangaa kitendo hicho kinashindikana na hatimaye ukaelekea moja kwa moja kwa Toby Alderweireld na kumgonga na kisha kujaa wavuni.

“Tukio kama hilo linatokea na inakuwa bahati kwa wapinzani katika dakika kama hizo, mchezo haukuwa rahisi, tulikuwa nyuma, lakini tuliweza kupambana na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha kabla ya wao kuongeza bao hilo katika dakika za mwisho.

“Imetuumiza kwa upande wetu, hivyo natumia nafasi hii kuomba radhi kwa kile kilichotokea, lakini ni jambo ambalo linatokea katika soka,” alisema mlinda mlango huyo.

Hata hivyo, kocha wa timu hiyo Mauricio Pochettino, amewataka wachezaji wake kusahau matokeo hayo dhidi ya Liverpool na kuangalia maandalizi ya mchezo mwingine dhidi ya wapinzani wao Crystal Palace, mchezo ambao utapigwa kesho kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wao mpya ambao utakuwa unafunguliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles