26.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Nchi sita kushiriki mafunzo ya usalama wa mionzi nchini

Mwandishi Wetu, Arusha

Wataalamu  25 wa Ulinzi  na Usalama  wa vyanzo  vya mionzi  kutoka nchi sita za Afrika, wanashiriki katika mafunzo ya wiki mbili  ya utoaji mafunzo ya ulinzi  na usalama wa vyanzo vya mionzi  yanaoendeshwa  na Umoja wa Ulaya kwa ushirikiano na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, Peter Ngamilo, amesema  mafunzo  hayo  yanayofanyika jijini Arusha yana lengo la kuwapatia ujuzi wakufunzi hao namna ya kufundisha wataalamu  mbali mbali wanaohusika na  usalama wa vyanzo vya mionzi katika nchi zao.

“Baada ya mafunzo hayo, wakufunzi hao watakuwa na uwezo wa kuchukua nafasi ya kuongoza katika mafunzo kwa wafanyakazi wa kitaifa katika nchi zao katika kuhakikisha kuwa vyanzo vya mionzi vinatumika  katika njia zilizo salama na halali.

“Vyanzo vya mionzi visipodhibitiwa vinaweza kutumika na katika vitendo vya kigaidi na kuleta madhara makubwa kwa jamii na kuathiri shughuli za maendeleo na uchumi,” amesema.

Pamoja na mambo mengine pia amesema washiriki watapata fursa ya  kufundishwa na kubaini usafirishaji haramu wa vyanzo vya mionzi hasa kwa wataalamu wa mamlaka za ulinzi na usalama ikiwamo Polisi, Walinzi waliopo mipakani  na wasimamizi wa teknolojia ya nyuklia, maofisa wa forodha na wataalamu wa kupambana na majanga ya nyuklia.

Pia, Ngamilo ametaja nchi wanazotoka washiriki hao kuwa ni Burundi, Uganda, Congo (DRC), Zambia, Ghana na wenyeji Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,631FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles