26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Kiongozi wa mbio za mwenge agoma kuzindua mradi wa maji

Samwel Mwanga, Bariadi

Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa, Mzee Mkongea Ali, amegoma kuzindua mradi wa ujenzi wa miundo mbinu ya usambazaji maji katika mitaa ya Nyaumata na Sesele halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu kwa madai kuwa kiasi cha fedha milioni 40 zilizotengwa katika
kupimia vifaa vya ujenzi wa mradi huo kutotumika kama ilivyopangwa.

Akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa mradi huo leo Mei 25 mjini hapo, amesema vipimo vya nondo vilivyotumika katika ujenzi wa tenki la kusambaza maji
havijaonyeshwa katika andiko la mradi licha ya fedha kiasi hicho kuonyesha zimetumika kwa ajili ya vipimo vya vifaa hivyo.

“Shilingi Milioni 40 zilitakiwa zitumike kwa ajili ya vipimo vya nondo
lakini utaratibu umekiukwa hivyo TAKUKURU shughulikieni na
watakaobainika wachukuliwe hatua kwani mradi huo umelenga kunufaisha
wananchi wa maeneo hayo.

kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo, Festo Kiswaga, ameiagiza TAKUKURU wilayani humo kumkamata na kumhoji mhandisi wa halmashauri hiyo, Mhandisi Moses Mwampunga na tuhuma hizo zikithibitika apelekwe mahakamani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles