26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Kiongozi CCM atibuana na mgombea Chadema

Benson-KigailaNA DEBORA SANJA, DODOMA

KATIBU wa Uchumi na Fedha wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dodoma, Rashid Morama, juzi alizua hali ya kutoelewana kati yake na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Benson Kigaila.

Tukio hilo lilitokea juzi katika kituo cha kupigia kura mjini Dodoma, baada ya Morama kuingia kituoni hapo akiwa na waangalizi wawili wa uchaguzi kutoka nje ya nchi.

Kabla ya hali hiyo kutokea, Kigaila aliingia kituoni hapo akisema alipata taarifa za uwepo wa kiongozi huyo wa CCM kutoka kwa watu wake wa karibu.

Baada ya kuingia kituoni hapo, hali ya utulivu ilitaka kutoweka, hali iliyowalazimu askari polisi waliokuwa kituoni hapo kuingilia kati.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya kituo hicho, Kigaila alisema alipigiwa simu na mawakala wakimwambia uwepo wa Morama ndani ya kituo hicho.

“Kwa mujibu wa sheria wanaotakiwa kuingia ndani ya kituo ni mawakala, wasimamizi wa uchaguzi, waangalizi wa uchaguzi na maofisa wa tume.

“Huyu humu ndani alifuata nini, maana tunasikia amekuwa akitembelea vituo, anatafuta nini?” alihoji Kigaila.

Nao polisi waliokuwa kituoni hapo walisema bila kutaja majina yao, kwamba hawakujua kama mwana CCM huyo siyo mhusika kituoni hapo.

 

Kigaila aliwalaumu Polisi huku akitaka kumpiga Morama pamoja na kurushiana maneno.

Licha ya Polisi kuingilia kati, hali hiyo ilidumu kwa dakika kadhaa kabla ya Morama kupanda gari lake na kuondoka akiwa na waangalizi hao wa uchaguzi, huku Morama akidai kwamba yeye alikwenda pale kama dereva wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles