28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kina Sheikh Faridi wagoma kula gerezani

Kiongozi-wa-Kikundi-cha-Uamsho-cha-Mjini-Zanzibar-Sheikh-Farid-Hadi-AhmedNa Kulwa Mzee, Dar es Salaam
KIONGOZI wa Uamsho na Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, Sheikh Faridi Hadi Ahmed na wenzake 22 wanaokabiliwa na tuhuma za ugaidi wamegoma kula gerezani.

Washtakiwa hao wamegoma kula na wamedai mahakamani kwamba hata waitwe wahaini hawawezi kugeuza madai yao ya kutaka Zanzibar ipate mamlaka yake kamili.

Hayo yalidaiwa jana na washtakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Renatus Rutta, wakati kesi yao ilipokuwa inatajwa.

Upande wa Serikali ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Janeth Kitali ulidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika hivyo ukaomba kesi iahirishwe huku ukisubiri kumbukumbu za mahakama kwa ajili ya kukata rufaa.

Mshtakiwa Sheikh Farid, alidai chanzo cha kushtakiwa katika kesi hiyo ni madai yao katika mchakato wa katiba ya kuhakikisha Zanzibar inapata mamlaka sahihi.

“Sisi wote ni viongozi wa jumuiya, baada ya yote hayo ndiyo misukosuko ikaanza kwetu, kesi ya ugaidi ni bandia, madai yetu hatuwezi kuyageuza hata watuite wahaini.

“Tulifanyiwa mambo mengi ya ukatili, sisi tunadai heshima ya nchi yetu, tulitamka wazi hatutaki Muungano tunataka Rais wetu apewe heshima yake kama Rais wa Zanzibar,” alidai.

Alidai hawana ajenda ya siri, walifanya mihadhara zaidi ya 200 na walitakiwa kushtakiwa Zanzibar kwa hiyo kutengeneza mazingira hayo ni kutaka kuwadhulumu haki zao.

Sheikh Faridi alidai Serikali iliyopo madarakani imezeeka na ni kikongwe.

Mshtakiwa huyo na wenzake 22 waliomba siku saba kesi yao isikilizwe na endapo zitaisha hatua watakayochukua itaonekana.

Alisema hawawezi kukubali kudhulumiwa huku wakikaa kimya. Walimtaka Kamishna wa Zanzibar ajieleze kwa nini aliamua kuwaleta Tanzania Bara kuwashtaki.

Hakimu Rutta alisema ni haki kwa waliopo gerezani kutembelewa, waliogoma kula waambiwe wale kwa sababu rai yake ni kujtaka wafike mahakamani na wanafuatilia kwa karibu.

Baada ya Hakimu kusema hayo kesi iliahirishwa hadi Mei 25 mwaka huu.
Mshtakiwa Salum Ally aliomba wapigwe risasi kichwani wamalizwe kwa sababu wamechoka.

Washtakiwa hao wanadaiwa kula njama kufanya ugaidi, kuwawezesha watu kufanya ugaidi na kuwahifadhi magaidi. Uhalifu huo unadaiwa ulifanyika sehemu mbalimbali ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles