Na ODACE RWIMO,
MKUU wa Wilaya ya Urambo,  Angelina Kwingwa, amemwagiza Mganga Mkuu wa Hospitali ya wilaya hiyo,  Heri Kagya,  kumchukulia hatua za nidhamu muuguzi, Samwel Andrew aliyetelekeza mgonjwa katika wodi ya wanaume kwa kutompatia matibabu kwa wakati.
Agizo hilo alilitoa juzi alipotembelea hospitalini hapo katika
maadhimisho ya Siku ya ya Ukimwi Duniani.
DC aliwatembelea wagonjwa katika wodi mbalimbali na kuwagawia misaada ya sabuni na juisi vilivyotolewa na Kikundi cha Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi wilayani humo.
Akiwa katika wodi ya wanaume, DC Â Kwingwa alisikitishwa na malalamiko
yaliyotolewa na mgonjwa, Â Ezekiel Kasuka (86), aliyeshutumu kitendo
cha muuguzi kumtelekeza akiwa amewekewa chupa ya maji  mkononi ambayo baadaye ikachomoka.
Inaelezwa kuwa  muuguzi huyo alimwacha hivyo  hivyo hivyo  kwa siku mbili hadi DC alipofika wodini humo.
Kwingwa  alisikitishwa zaidi na kitendo cha muuguzi huyo kumwambia
mgonjwa akanunue dawa yeye mwenyewe nje ya hospitali wakati hali yake
haikuwa nzuri.
Baada ya kuonyeshwa muuguzi aliyelalamikiwa na mgonjwa huyo na kutakiwa kueleza sababu za kumtelekeza, Andrew  alisema hakuwa
na dawa ya kumwongezea ndiyo maana alimwomba mgonjwa akanunue mwenyewe.
DC alilikataa jibu hilo ikizingatiwa  hata dawa ya mwanzoni haikuisha
kwa chupa ya maji  ilichomoka na kuachwa  hivyo hiyo.
Mzee Kasuka alimwambia DC kuwa alifika hospitalini hapo Novemba 30,
mwaka huu  saa 9.00 alasiri na kupewa kitanda  na alianza kuhudumiwa jioni ya Novemba 31.
Alieleza kuwa huduma aliyopewa ilikuwa ni kuwekewa  dripu ya maji  lakini
baada ya muda kidogo sindano ilichomoka.
Kasuka alisema  kwa vile alikuwa hana msaidizi aliomba msada kutoka kwa muuguzi bila mafanikio na alipoingia wodini humo aliamua kuitoa na kweka pembeni na kurejea ofisini kwake.
Mganga Mkuu, Hery Kagya, alisema kitendo kilichofanywa na muuguzi
huyo ni uzembe wa hali ya juu na kuahidi kuchukua hatua stahiki kwa
mtumishi huyo.
Mkurugenzi Mtendaji, Magreth Nakainga, alisema mludikano wa wagonjwa
hospitalini hapo unatokana na wilaya jirani ya Kaliua kutokuwa na
hospitali ya wilaya hivyo wagonjwa hilazimika kwenda katika hospitalini hapo huku
wengine wakitokea wilaya za Sikonge, Uyui na Uvinza.