24.3 C
Dar es Salaam
Monday, September 16, 2024

Contact us: [email protected]

Kikokotoo mafao ya wastaafu sasa asilimia 40

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Serikali imetangaza kuongezeka kwa malipo ya mkupuo kwa wastaafu kutoka asilimia 33 hadi asilimia 40 kwa kundi la watumishi walioshushwa kutoka asilimia 50 hapo awali.

Kwa muda mrefu wafanyakazi walikuwa wakilalamikia kikokotoo cha pensheni za wastaafu kinachotumika kutokidhi hali halisi ya wanachama wakitaka kurejeshwa kwa kanuni za zamani zilizotumika kabla ya mwaka 2017.

Msimamo huo mpya umetangazwa leo Juni 13,2024 na Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, wakati akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka wa fedha 2024/2025.

Amesema wastaafu waliokuwa wakipokea asilimia 25 hadi 33 sasa watapandishwa hadi asilimia 35 na walioathirika na mabadiliko yaliyojitokeza watakuwa sehemu ya mabadiliko hayo.

“Serikali imesikia kilio cha watumishi na kufanyia kazi suala la masilahi ya wastaafu, Rais Samia ameelekeza kuongezeka kwa malipo ya mkupuo kutoka asilimia 33 hadi asilimia 40 kwa kundi la watumishi walioshushwa kutoka asilimia 50 hapo awali.

“Serikali itaendelea kuliangalia kwa karibu suala la masilahi ya wastaafu kwa kuzingatia tathmini ya uhai na uendelevu wa mifuko yetu,” amesema Dk. Mwigulu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles