Kifafa chamwangusha Lil Wayne

Lil Wayne
Lil Wayne

WISCONSIN, MADISON

RAPA Lil Wayne, ameendelea kusumbuliwa na ugonjwa wa kifafa baada ya juzi kuanguka akiwa kwenye ndege.

Msanii huyo alikuwa ndani ya ndege akitokea mji wa Wisconsin akielekea California akaanguka na kupoteza fahamu. Hata hivyo, ndege hiyo ilitua kwa dharura kwa ajili ya kumsaidia msanii huyo akimbizwe hospitalini.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, msanii huyo mwenye umri wa miaka 33 alishushwa kwenye uwanja wa ndege wa Omaha mjini Nebraska kwa ajili ya matibabu.

Hata hivyo, wakati anakimbizwa hospitalini alizinduka na kukataa kupelekwa hospitali huku akitaka aendelee na safari, baada ya kupanda kwenye ndege lakini dakika mbili baadaye alipatwa tena na tatizo hilo madaktari wakamhudumia humo humo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here