25 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

KIFAA KIPYA CHA KUPIMIA UGONJWA WA SELIMUNDU CHAZINDULIWA

sickle-scanKifaa kipya cha kupima vinasaba vya ugonjwa wa selimundu kiitwacho sickle scan, ambacho kinapima na kutoa majibu ndani ya dakika tano, kimezinduliwa nchini.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangwala, kifaa hicho kimeagizwa na kuletwa nchini na Kampuni ya Medomix kwa lengo la kupanua huduma zitakazosaidia kubaini aina mbalimbali za selimundu kwa wagonjwa.

Kipimo hicho ambacho kitatoa majibu ndani ya muda mfupi, kina uwezo wa kufanya kazi kwenye mazingira yoyote hata bila ya kutumia umeme hivyo kitasaidia pia kupunguza gharama.

Alisema takwimu zinaonesha kila mwaka duniani watoto 312,307 huzaliwa wakiwa na ugonjwa wa selimundu ambapo asilimia 76 ni kutoka barani Afrika hii ni sawa na watoto 237,253.

“Kwa Tanzania ni kati ya watoto 8,000 hadi 11,000 huzaliwa na selimundu kati yao asilimia 15 hadi 18 ni ‘traits’, kwa Afrika nafasi ya watoto wenye ugonjwa huo kuishi ni asilimia 50 na kwa nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara ni asilimia 10,” alisema.

“Mwishoni mwa mwaka jana tuliwapima watoto 3,981 katika Hospitali ya Temeke na Muhimbili, asilimia 0.77 walikuwa tayari ni wagonjwa wa selimundu, asilimia 12.7 walikutwa na vinasaba,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles