22.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

MSD: HOSPITALI ZISIZOLIPA MADENI HAZITAPATA DAWA

mkurugenzi-mkuu-wa-msd-laurean-bwanakunu
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu

Bohari Kuu ya Dawa nchini, (MSD) imesema hospitali zote zisizolipa madeni zikiwamo teule na za serikali hazitapata dawa.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu amesema hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana hali ya upatikanaji wa dawa nchini ilikuwa ya kuridhisha.

“Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu aina 17 za dawa zitawasili na hali ya dawa inategemewa kwa asilimia 86, Februari mwaka huu aina tatu za dawa zitawasili jambo ambalo litasaidia kuboresha hali ya upatikanaji wa dawa kwa asilimia 88.

“Ni matazamio yetu kuwa hadi kufikia machi mwaka huu aina mbili za dawa zitawasili nchini jambo ambalo tunatarajia kuwa litaongeza kiwango cha upatikanaji wa dawa kwa asilimia 90,” alisema Bwanakunu.

Alisema hali hiyo imefanya kuwepo kwa aina 100 za dawa kati ya 135 ya dawa zote muhimu.

Aidha alisema msd imeanzisha mchakato wa kuanzisha viwanda vya kuzalisha dawa na vifaa tiba nchini  kupitia mpango ushirikishwaji wa sekta binafsi  ili kupunguza gharama  za kuagiza dawa nje ya nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles