24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

Kichuya aingia rada za Ajib

KichuyaNa ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM

WINGA wa timu ya Simba, Shiza Kichuya, ameanza kusaka rekodi ya mshambuliaji wa kikosi hicho, Ibrahim Ajib, baada ya bao lake kuingia katika rekodi.

Kichuya aliyejiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro, alifunga bao hilo akimalizia kona ya Mohamed Hussein kwa shuti kali katika mechi yao ya Ligi Kuu dhidi ya Ndanda FC wiki iliyopita katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Wekundu hao wa Msimbazi kushinda mabao 3-1.

Mmoja wa watu waliopo ndani ya Bodi ya Ligi, inayosimamia ligi hiyo ameliambia MTANZANIA Jumamosi kuwa bao hilo tayari limewekwa kwenye orodha ya mabao bora ya msimu wa 2016/17.

Alisema kama ilivyo kawaida, baada ya mechi kumalizika kunakuwa na taarifa zinazopelekwa bodi ya ligi pamoja na kuangaliwa kwa video ili kujiridhisha kama mechi ilichezeshwa kwa haki na hapo ndipo ilipoonekana bao la Kichuya linastahili kuwa miongoni mwa mabao bora ya msimu.

“Mara baada ya Kichuya kufunga bao hilo, viongozi wa bodi ya ligi walianza kuzungumza juu ya ubora wake, lakini walijiridhisha baada ya kumalizika mechi katika utaratibu wa kuangalia marudio ya mechi na hivyo kwa pamoja tukakubaliana bao hilo liingie kwenye orodha ya mabao bora ya msimu,” alisema.

Katika msimu uliopita wa ligi, Ajib alifunga bao dhidi ya Mgambo Shooting na Amissi Tambwe, alifunga kwenye mechi dhidi ya Mbeya City na kuingia katika kinyang’anyiro hicho ambacho Ajib aliibuka kidedea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles