23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Khimji aipongeza Ama’z kujali afya za wafanyakazi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Saady Khimji, ameipongeza Kampuni ya Ama’z Auction Mart kwa kubuni mbinu ya kuandaa mashindano ya mpira kwani yanajenga afya za wafanyakazi.

Wafanyakazi wa Kampuni ya Udalali ya Ama’z wakichuana wakati wa bonanza maalumu lililofanyika kwenye uwanja wa Jakaya Kikwete. Katika bonanza hilo timu ya Camp iliibuka kidedea kwa kuifunga timu ya Noah mabao 6.

Akizungumza wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika Uwanja wa Jakaya Kikwete, Khimji ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema magonjwa mengi hasa yasiyoambukiza ni matokeo ya mtindo mbaya wa maisha.

“Siku hizi kuna matatizo ya presha, kisukari na magonjwa mengine lakini wataalam wa afya wanatuambia sababu kubwa ni mtindo mbaya wa maisha, hivyo niwapongeze Ama’z kwa hiki mlichokifanya siyo tu kwa sababu mna furaha ya kutimiza mwaka mmoja lakini mnajali afya za wafanyakazi wenu,” amesema Khimji.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Ama’z Auction Mart, Dawa Jumanne, amesema waliandaa mashindano hayo kuadhimisha mwaka mmoja tangu walipozindua kampuni hiyo mwaka jana.

“Mikakati ya Ama’z ni kuendelea kuboresha huduma za udalali na huduma nyingine kupitia kampuni yetu ya usafi ili tufikie malengo tuliyojiwekea ya kutoa huduma bora kwa jamii,” amesema Dawa.

Mratibu wa mashindano hayo Rashidi Msangi, amesema yalihusisha timu za kampuni hiyo ambapo vijana wa Camp waliibuka washindi kwa mabao 6 – 0 dhidi ya wenzao wa Noah na kuzawadiwa mbuzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles