26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

KESI ZA MTANDAO 7,899 ZIKO MAHAKAMANI

Tangu kuanza kutumika kwa sheria ya mtandao (Cyber Act) jumla ya kesi 7,899 za makosa hayo zimefikishwa mahakamani katika kipindi cha mwaka 2015/2016 huku makosa ya kutoa taarifa za uongo zikiongoza.

Mrakibu Msaidizi wa Polisi kutoka Kitengo cha Uhalifu wa Mtandao, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Joshua Mwangasa amesema kati ya Januari hadi Juni mwaka huu, kesi zilizofikishwa mahakamani ni 3,346.

“Maendeleo ya kesi ni mazuri na nyingine tunaelekea kushinda, lakini akaunti ambazo hazijulikani zinaleta shida katika upelelezi. Tunaendelea kufanya ‘online patrol’ ili kuhakikisha mitandao inatumika kwa usalama,” amesema Mwangasa.

Kwa mujibu wa ofisa huyo watu wengi wamekuwa wakifanya makosa bila kujua, kutafuta umaarufu huku wengine wakifanya kwa lengo la kujipatia kipato.

Pamoja na mambo mengine, amewataka wamiliki wa mitandao ya kijamii kuhakikisha wanakuwa na sera ili kuhakikisha kila anayefungua akaunti anajulikana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles