Cape Town, Afrika Kusini
Mahakama kuu nchini Afrika kusini leo Mai 26, 2021 inatarajiwa kuanzia kusikiliza kesi ya aliyekuwa Rais wa zamani wa Taifa hilo Jacob zuma dhidi ya tuhuma za ufisadi.
Rais Zuma anatarajiwa kukana mashtaka ya udanganyifu na ulaghai katika kesi ambayo ilianza na mkataba wa mauziano ya silaha miaka ya 1990.
Pia Zuma anakabiliwa na madai mapya ya ufisadi na huenda akafungwa jela kwa kukiuka amri ya mahakama katika kesi nyingine tofauti.
Raia wa afrika kusini wanaamini kesi hiyo inaweza kuashiria mabadiliko ya nchi hiyo.
Baadhi ya mashujaa wa ukombozi wa uhuru nchini Afrika Kusini wamemshutumu Jacob Zuma na kuonya itachukua muda mrefu kurekebisha uharibifu alioufanya dhidi ya taasisi changa za nchi.