27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

KESI YA VIGOGO TRL KUANZA KUSIKILIZWA

Na KULWA MZEE -DAR ES SALAAM


 

2-2

KESI inayowakabili vigogo 11 wa Mamlaka ya Reli Tanzania (TRL) ya matumizi mabaya ya madaraka kwa kukiuka sheria wakati wa ununuzi wa mabehewa 25 inatarajiwa kuanza kusikilizwa Desemba 5, mwaka huu.

Kesi hiyo ilikuja jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa, kwa ajili ya kuanza usikilizwaji wa awali.

Wakili kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Magala Ndimbo, akisaidiana na Max Ally, alidai mahakamani kwamba walikuwa tayari kwa kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali dhidi ya mashtaka yanayowakabili.

Wakili wa utetezi, Ambrose Malamsha, aliomba kesi hiyo iahirishwe kwa sababu maelezo wamepewa baada ya kuingia mahakamani na washtakiwa wawili hawana wawakilishi.

Hakimu Nongwa alikubali kuahirisha kesi hiyo hadi Desemba 5, mwaka huu, mawakili wa washtakiwa wanatakiwa kuwepo.

Vigogo hao ni  Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Kipallo Kisamfu, Mkuu wa Kitengo cha Makenika na Mhasibu Mkuu Jasper Kisiraga, Kaimu Meneja wa Usafiri, Mathias Massae, Kaimu Mhandisi wa Ufundi na Meneja Ujenzi, Muungano Kaupunda na Mkuu wa Ufundi na Meneja Ujenzi, Ngoso Ngosomwiles.

Wengine ni Mhandisi Mkuu wa Ufundi, Paschal Mafikiri, Mhandisi Mipango Kedmo Mapunda, Kaimu Mhandisi wa Mawasiliano, Felix Kashaingili, Mkuu wa Usafiri wa Reli, Lowland Simtengu; Mkuu wa Ubunifu na Utengenezaji wa Nyaraka, Joseph Syaizyagi na Kaimu Mkuu wa Usafirishaji; Charles Ndenge.

Katika hati ya mashtaka inadaiwa kuwa kati ya Februari Mosi 2013 na Juni 30, 2014, katika Makao Makuu ya TRL, Kisamfu akiwa mfanyakazi wa mamlaka hiyo, alitumia vibaya madaraka yake kwa kushindwa kusimamia vizuri zabuni kama ilivyokuwa inatakiwa kwenye vigezo na masharti.

Inadaiwa kuwa, tukio hilo ni kinyume cha Sheria namba 21 ya Manunuzi ya 2004, jambo lililoipa faida kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and Industries Limited.

Upande huo wa Jamhuri ulidaiwa kuwa, kati ya Julai mosi na Agosti 31, 2013, Mafikiri alitumia madaraka yake vibaya kwa kuidhinisha michoro iliyoandaliwa na M/S Hindusthan, jambo ambalo ni kinyume cha vigezo na masharti ya zabuni.

Pia, Kaupunda anadaiwa alitumia madaraka vibaya kwa kuruhusu kutengenezwa kwa mabehewa 25, bila kuzingatia vigezo na masharti ya zabuni hiyo.

Katika mashitaka mengine, Kisiraga na Massae, wanadaiwa Agosti 5, 2014, walitumia madaraka vibaya kwa kuidhinisha malipo ya Dola za Marekani milioni 1.3 bila kuthibitisha matumizi ya mabehewa 25, kupitia Cheti cha Ukaguzi na cha kukubali kinachotolewa na TRL, baada ya kufanyiwa majaribio, jambo ambalo ni kinyume cha Sheria na kanuni za manunuzi.

Ilidaiwa kuwa, kati ya Januari Mosi na Februari 2014, washtakiwa Kaupunda, Mapunda, Kashaigili, Simtengu na Syaizyagi, wakiwa wajumbe wa bodi ya zabuni,  walitumia madaraka yao vibaya kwa kuiruhusu M/S Hindusthan kushinda, ambayo ilikuwa haijakidhi vigezo kushinda zabuni hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles