25.8 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kero ya maji Kinondoni mbioni kumalizika

KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godfrey Chongolo amewaondoa hofu wananchi wilayani kwake kwa kuwaahidi kwamba kero ya maji iko karibu kumalizika na kwamba hakutakuwa na malipo ya fidia katika maeneo yanapopita mabomba.

Chongolo amesema hayo leo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mbopo.

“Tuambiane ukweli, fidia hakuna, ukigomea njia maana yake umezuia tusipeleke maji kwako na kwa wengine, tutafidia barabara na vingine,” amesema Chongolo.

Anasema fedha zipo, Dawasa hivyo  mkandarasi akikamilisha mchoro kazi inaaanza.

“Julai mwaka jana Rais John Magufuli alitoa Sh. bilioni 74 kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya maji jijini Dar es Salaam ikiwemo Kinondoni kwa kilomita 1500, wenyeviti wote wa vitongoji walitia saini mkataba,” alisema Chongolo.

Amesema Julai mwaka jana walisaini mkataba na mkandarasi, kilomita 1500 za ulazaji wa bomba.

Mkandarasi yuko katika hatua za mwisho za kutambua njia za kupitia bomba, ameweka alama, ataanza kujenga mtandao.

Pamoja na barabara pia ameahidi kumaliza changamoto ya umeme na kuboresha barabara za vumbi ili zipitike.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles