24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

ACT Wazalendo yapokea wanachama 176 kutoka CUF

Amina Omari, Tanga

Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Shariff Hamad amepokea jumla ya madiwani watano na wanachama 176 kutoka Chama cha CUF kutoka wilaya za Tanga na Pangani.

Wanachama hao wamepokelewa leo wakati wa ziara ya siku moja ya Mwenyekiti huyo mkoani Tanga iliyoenda sambamba na uzinduzi wa matawi matatu.

Aidha akiongea na wanachama wa Chama hicho aliwataka kuhakikisha wanajiandaa kwa ajili ya kushinda uchaguzi mkuu ujao kuanzia ngazi ya kata hadi urais.

“ACT ndio chama pekee kilichobaki ambacho kitaweza kuleta ukombozi kwa Watanzania kwa sasa “amesema Maalim Seif.

Huku akiitaka serikali kuhakikisha inakuwa na tume huru ya uchaguzi ambayo haifungani na dola ili iweze kutenda haki tofauti na ilivyosasa.

“Tanzania ili tuweze kuendelea tunahitaji kuwa na dola huru ambayo haifungamani na matakwa ya chama “amesitiza Mwenyekiti huyo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,310FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles