NAIROBI, Kenya
MWANAMUME moja ameshtakiwa kwa tuhuma za kudukua mfumo wa kifedha wa Mamlaka ya Mapato ya Kenya (KRA).
Udukuzi huo unadaiwa kusababisha mamlaka hiyo kupoteza jumla ya Sh bilioni 4 za Kenya ambayo ni sawa na Dola za Marekani milioni 39.
Kwa mujibu wa taarifa ya BBC, Alex Mutunga Mutuku, alishtakiwa makosa ya kutekeleza ulaghai kwa kutumia mifumo ya kielektroniki.
Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa Mutuku alikuwa sehemu ya mtandao mkubwa wa watu waliokuwa wakiiba pesa kutoka kwa taasisi na kampuni kubwa nchini humo.
Alidaiwa kutekeleza makosa hayo kati ya Machi 2015 na Machi mwaka huu.
Gazeti la Standard lilisema kuwa, wakili wa upande wa mashtaka Edwin Okello aliambia mahakama: "Sakata hii ni kubwa na inahusisha hata watu walio nje ya nchi” alisema.