25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Kayandambila ahimiza uandikishaji wa wanafunzi shule shikizi Muleba

Na Renatha Kipaka, Muleba

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, Elias Kayandabila ametembelea shule shikizi zilizojengwa kwa fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko-19 ili kuona hali ya uandikishaji wa watoto wanaojiunga na masomo ya awali na darasa la kwanza.

Akizungumza hivi karibuni na Wazazi waliowaleta wanafunzi kuanza masomo ya awali katika shule Shikizi ya Daraja Nane, iliyopo kijiji cha Kiziramuyaga, Kata ya Kimwani, Kayandambila amewasihi kupeleka watoto shule .

Amesema lengo la kufanya hivyo ni kuwaelimisha wazazi wenzao ambao bado hawajapeleka watoto wao shule nakwamba elimu ni urithi kwa watoto wao.

“Nafurahi kuona mmekuwa na mwitikio mzuri wa kuwaleta watoto shule, kwa shule shikizi ya Daraja Nane maoteo ilikuwa ni kuandikisha watoto wa shule ya awali 208 na mpaka sasa wameandikishwa watoto 128, hali hii inatia moyo,” amesema Kayandambila.

Ninafurahi shughuli na ujenzi zinazoendelea katika shule hiyo na kuwaeleza kuwa Halmashauri imetoa kiasi cha Sh milioni 6.6 kwa ajili ya umaliziaji wa vyoo huku akiwasihi wazazi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kukamilisha miundombinu mingine inayotakiwa katika shule hiyo kama nyumba za walimu.

Naye, Joseph Mathias mmoja wa wazazi aliyefika shuleni hapo kwa ajili ya kumuandikisha mwanaye, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuona uhitaji wa jamii na kuwashika mkono kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule shikizi ambapo awali watoto wao walikuwa wakisoma katika mazingira yasiyoridhisha jambo ambalo limewasaida watoto wao kusomea katika madarasa bora na ya kisasa.

“Nitumie Frusa hii kuwashukuru viongozi wa wilaya ya Muleba kwakujituma mpaka kukamilisha ujenzi wa madarasa maana sio rahisi “amesema Mathias.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles