24.3 C
Dar es Salaam
Monday, September 16, 2024

Contact us: [email protected]

Kaya 1,373 zenye watu 8,364 na Mifugo 36,457 zahama kwa hiari ngorongoro

Na Kassim Nyaki, Dodoma.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amelieleza bunge kuwa jumla ya kaya 1,373 zenye watu 8,364 na mifugo 36,457 zimehama kwa hiari katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro kwenda kijiji cha msomera Mkoani Tanga na maeneo mengine.

Waziri Kairuki ametoa taarifa hiyo wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii Bungeni jijini Dodoma leo tarehe 31 Mei, 2024 na kueleza kuwa Serikali kupitia Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imeendelea kuhamasisha wananchi wanaoishi ndani ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kujiandikisha kuhama kwa hiari kwenda katika maeneo yaliyotengwa na Serikali ambayo ni Msomera-Handeni, Saunyi-Kilindi, Kitwai-Simanjiro na maeneo mengine ambayo wananchi wanayoyachagua wenyewe.

Mhe. Kairuki ameongeza kuwa tangu zoezi hilo lilipoanza mwezi juni 2022 hadi Aprili 2024, jumla ya Shilingi 286,681,137,369 zimetolewa na Serikali kuwezesha utekelezaji wa zoezi hilo ambalo kwa sasa lipo awamu ya pili.

Katika awamu ya kwanza iliyoanza juni 2022 hadi januari 2023, jumla ya kaya 551 zenye watu, 3010 mifugo 15,321 zilihama ndani ya hifadhi kwenda Msomera na maeneo mengine ambapo Nyumba zaidi ya 500 zilijengwa katika kijiji cha Msomera na wananchi kuhamia.

Mhe. Waziri amefafanua kuwa Katika awamu ya pili ya utekelezaji wa zoezi hilo, jumla ya nyumba 1,000 kati ya nyumba 5,000 zinazojengwa (Msomera nyumba 2,500; Saunyi nyumba 1,000 na Kitwai nyumba 1,500) zinazotarajiwa kujengwa zimekamilika.

Vilevile, nyumba 1,500 zipo katika hatua mbalimbali za ujenzi katika Kijiji cha Msomera (hatua ya bati – nyumba 600, hatua ya Lenta nyumba 260 na hatua ya usawa wa madirisha nyumba640).

Waziri Kairuki amebainisha katika awamu ya pili ya zoezi hilo lililoanza mwezi agosti 2023 hadi kufikia tarehe 28 aprili, 2024, jumla ya kaya 822 zenye watu 5,354 na mifugo 21,136 zimehama kwa hiari.

Kwa ujumla tangu zoezi hilo lilipoanza mwezi juni 2022 hadi mwezi aprili, 2024 jumla ya Kaya zilizohama kwa hiari ni katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro ni kaya 1,373 zenye watu 8,364 na mifugo 36,457 huku zoezi la uelimishaji, uandikishaji, uthaminishaji na uhamishaji likiendelea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles