27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Katiba mpya kichwa chini miguu juu

Bunge
Bunge

NA MWANDISHI WETU, DODOMA

MJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba, Ali Omar Juma, amewalalamikia wajumbe walio wengi, kwamba hawawatendei haki Watanzania kwa kuwa wanaandaa mazingira ya kupata Katiba ya upande mmoja.

Juma alitoa shutuma hizo jana alipokuwa akiwasilisha maoni ya wachache katika kamati namba nne.

Katika mazungumzo yake, alisema kitendo cha kundi la walio wengi kuandaa mazingira ya kutunga Katiba inayopingana na mapendekezo ya Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, hakiwezi kukubaliwa na Wazanzibari kwa kuwa kinakwenda kinyume na matarajiio yao.

“Kitendo cha kujadili maoni ya Serikali mbili wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipendekeza Serikali tatu siyo cha kistaarabu.

“Mheshimiwa Makamu Mwenyekiti, kinachojadiliwa sasa hapa Dodoma ni Katiba ya Tanganyika na siyo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Kwahiyo, nawaambia kama Katiba itapatikana kwa mtindo huu, haitakuwa Katiba ya kutumika Zanzibar, hii itakuwa ni Katiba ya Tanganyika na mwisho wake utakuwa Kisiwa cha Chumbe.

“Lazima itaishia Chumbe kwa sababu hata marehemu Karume aliwahi kulikataa Azimio la Arusha na kusema liishie Kisiwa cha Chumbe na kweli ilikuwa hivyo,” alisema Juma.

Kuhusu kura za urais, aliwashangaa wajumbe wa kundi la wengi, waliopendekeza mshindi apatikane kwa wingi wa kura.

Kutokana na hali hiyo, aliwataka wajumbe wenzake wakubali mshindi wa nafasi ya urais apatikane baada ya kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura zilizopigwa.

Awali wakati akiwasilisha maoni hayo, baadhi ya wajumbe walionekana kulalamikia kauli zake kwa kile walichosema anatoa lugha zisizofaa.

Miongoni mwa waliolalamika na kutaka kutoa taarifa na kukataliwa na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samia Suluhu Hassan ni Paul Makonda ambaye ni kiongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM).

Wakati huo huo, Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Amour Arfi (Chadema) aliwalalamikia wajumbe wa Bunge hilo kwa kuwa wanatoa majibu mapesi katika maswali magumu.

Kutokana na hali hiyo, alisema pamoja na mjadala wa Bunge unaoendelea, hakuna uwezekano kupatikana kwa Katiba bora kwa kuwa utaratibu wa mijadala siyo unaotakiwa.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Wanaolalamikia mwenendo wa Bunge la Katiba mpya ni wanafiki maana UKAWA walipobaini ujanja wa CCM kujiundia katiba yake waliamua kutoka Bungeni mpaka sasa hawajarudi. Swali ni je, hawa wanaolalamika sasa kwa nini hawakuungana na UKAWA. Ni vyema waandishi wa habari wakaacha kuandika habari zao ili tuwape uwanja wa kutosha makada wa CCM waaandae Katiba Mpya wanayotaka wao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles