27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kapombe, Leonel waiua Azam Kagame

Kikosi cha Azam
Kikosi cha Azam

NA ZAITUNI KIBWANA, RWANDA

TIMU ya Azam FC jana imeaga Michuano ya Kombe la Kagame, baada ya kutolewa kwa mikwaju ya penalti 4-3 na timu ya El- Merreikh ya Sudan, katika mchezo wa robo fainali uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Nyamirambo, mjini hapa.

Mchezo huo ulifikia kuamuliwa kwa penalti baada ya timu hizo kwenda sare ya kutofungana ndani ya dakika tisini.

Wachezaji wa Azam waliopata penalti ni, Aggrey Morris, Didier Kavumbagu na Erasto Nyoni, huku Shomar Kapombe akipaisha na penalti ya Lionel Saint-Preux ilidakwa na kipa wa El- Merreikh, Magoola Omar.

Walioiwezesha El- Merreikh kutinga hatua ya nusu fainali ni Allan Wanga, Magdi Abdelatif, Ayman Mohamed na Alli Hussein wakati penalti ya Elbasha Ahmed ilipanguliwa na kipa Mwadin Ali Mwandin.

Katika mchezo huo, Azam walikuwa wa kwanza kulishambulia lango la El- Merreikh, ambapo John Bocco alishindwa kufunga dakika ya saba kufuatia krosi ya Aggrey Morris, baada ya shuti lake kuokolewa na kipa wa El- Merreikh, Omar.

El-Merreikh walifanya shambulio katika dakika ya 26, baada ya Elbasha Ahmed kutoa pasi kwa Traore Mohamed, lakini kipa wa Azam, Mwadin alipangua shuti lake.

Dakika ya 28, Azam walikosa bao baada ya shuti la mshambuliaji wa timu hiyo  Kipre Tchetche kugonga mwamba pasi ilitoka kwa Leonel Saint-Preux.

Baadaye Bocco akiwa yeye na kipa wa El-Merreikh, Omar alishindwa kumalizia pasi nzuri ya Kipre katika dakika 37 na mpira kutoka nje.

Katika dakika ya 60, Mohamed wa El-Merreikh aliwatoka mabeki wa Azam na kupiga shuti lakini alishindwa kulenga lango.

Azam walipoteza nafasi nyingine ya kufunga baada ya Kipre kupiga shuti kali, lakini lilitoka sentiminta chache kutoka langoni mwa El-Merreikh.

Dakika ya 75, Mohamed wa El-Merreikh alipiga shuti nje ya eneo la 18, lakini Mwadin alipangua.

Azam FC: Mwadin Alli Mwandin,  Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, David Mwantika, Aggrey Morris, Michael Bolou, Himid Mau, Salum Abubakari, John Bocco/ Didier Kavumbagu, Leonel Saint-Preux na Kipre Tchechte.

El-Merreikh: Magoola Omar, Albasha Ahmed, Bakhiet Mohamed, Ayman Mohamed, Ali Hussein, Wawa Pascal, Alla Yousif, Amir Kamal, Ramadhan Agab, Traore Mohamed na Gabir Mohamed.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles