30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Kampuni zajitokeza kufadhili mashindano ya Gofu Corperate Masters 2021

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kampuni mbalimbali nchini zimetakiwa kuendelea kushiriki katika mashindano ya Mchezo wa Gofu ikiwa ni moja ya sehemu ya kukutana na kubadilishana mawazo ikiwamo fursa za kibiashara.

Afisa Maendeleo ya Michezo wa Baraza la Michezo Taifa (BMT), Milinde Mahona akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya Gofu kwa Makapuni ya Kibiashara ya Corperate Masters 2021 yenye lengo la kujenga mahusiano na ushirikiano wa kibishara, katika viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam juzi. Kulia ni Kapteni wa Gofu, Fred Laizer. Kushoto ni Mwenyekiti wa mashindano hayo, Kelly Kariuki, Kulia ni Mchezaji wa Gofu Klabu ya Lugalo, Nathan Mpangala, Kapteni wa Gofu, Fred Laizer na Mdhamini wa mashindano kutoka Benki ya CRDB, Gibson Mlaseko.

Wito huo umetolewa juzi jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Corporate Masters Gofu Competition, Kelly Kairuki ambapo amesema mashindano hayo yanatoa fursa kwa wafanyakazi wa kampuni za kibiashara na wafanyabiashara kukutana na kubadilishana mawazo kuhusu biashara, uchumi huku wakicheza mchezo huo.

“Hii ni fursa kwa kampuni mbalimbali kutumia mashindano haya ya mchezo wa gofu yanayofahamika kama Corporate Masters Gofu Competition 2021, hivyo niwahimize kampuni nyingine kuonyesha ushiriki wao kwa ajili ya kusaidia kupata mawazo mapya ya kibishara kwa kupitia mchezo huu.

“Kwa mwaka huu mashindano haya yanatarajiwa kufikia kilele chake Agosti 7, katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, hivyo niwaombe wadau na wapenzi wa gofu kutoka kampuni na mashirika mbalimbali kujitokeza katika kilele hicho.

“Dhumuni la mashindano hayo ni kuwaleta pamoja mameneja na wafanyabiashara kukutana kucheza, kubadilishana mawazo, kutangaza biashara zao na kuwezeshana kama wafanyabiashara,” amesema Kairuki.

Mchezaji wa Gofu wa Klabu ya Gymkhana, Gulam Dewji, akipiga mpira wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Gofu kwa Makapuni ya kibiashara ya Corperate Masters 2021 katika viwanja vya Gymkhana Dar es Salaam juzi usiku.

Aidha, ameishukuru serikali kwa kusema kuwa; “Tunaishukuru serikali kwa kutuwezesha kuwa hapa na kutupa ushirikiano mkubwa. Aidha, tunawashukuru wadhamini wetu mbali mbali waliojitokeza kufanikisha mashindano haya,” amesema Kairuki.

Naye, Mdhamini Mkuu wa mashindano hayo, Gibson Mlaseko ambaye ni Meneja Mwandamizi wa huduma ya Primier wa Benki ya CRDB amesema mashindano hayo ni mazuri kwa sababu yanawakutanisha wafanyabiashara pamoja.

“Sisi kama Benki ya CRDB tunatoa ushirikiano katika michezo, lakini tumeona katika eneo hili la gofu ni eneo zuri linaleta wadau kutoka maeneo mbali mbali. Hivyo tumeona hii ni fursa adhimu ya kuweza kukutanisha watu kwa ajili ya kuweza kuboresha biashara zao,” amesema Mlaseko.

Akizungumizia maandalizi ya mashindano hayo, alisema yameandaliwa vizuri, ambapo wanategemea katika kilele chake itakuwa bora zaidi na ni fursa kwa wao kukutana na wadau wa sekta mbali mbali za uchumi na kuangalia namna watavyoweza kushirikiana na kuboresha thamani katika maeneo yao.

Awali, Afisa Maendeleo ya Michezo kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Milinde Mahona akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Hassan Abbas amesema michezo ni sehemu ambayo watu wanaweza kukutana na kupata marafiki wapya ambao wanaweza kufanya biashara.

Hivyo, ameziomba kampuni mbali mbali zijitokeze kufadhili michezo.

“Michezo ni fursa kubwa kwa wadau kuonesha namna wanavyoweza kuwa pamoja, nawapongeza pia wote waliojitokeza na waliojiunga na mchezo wa golf kutoka kampuni mbali mbali, ambapo serikali itaendelea kushirikiana kutoa ushirikiano katika michezo,” amesema Milinde.

Afisa huyo, amefafanua zaidi kuwa kampuni ambazo ziko kwenye Corporate Masters zisiishie kwenye gofu peke yake, badl yake yazidishe umoja na yaendelee kuona fursa zilizopo katika sekta ya michezo. 

Amesema kampuni zitumie fursa hiyo ili ziweze kujiendeleza kibiashara, lakini pia Watanzania waweze kunufaika na fursa ambazo kampuni hizo zitaonesha.

“Michezo ni fursa, kwa sababu kuna fursa za kibiashara, ambapo wanaweza kuanzisha ushirikiano katika viwanda kwa kuzalisha vifaa vya michezo na hata kampuni za kuuza vifaa vya michezo, kujenga miundombinu na kudhamini michezo mbali mbali itakayowawezesha kujitangaza,” amesema.

Mshiriki wa mashindano ya Gofu kwa Makapuni ya kibiashara ya Corperate Masters 2021, Subira Gudadi kutoka Benki ya CRDB, akipiga mpira wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo katika viwanja vya Gymkhana Dar es Salaam juzi usiku.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles