27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 12, 2024

Contact us: [email protected]

KAMPUNI YAKOPESHA WAKULIMA MBEGU ZA MILIONI 119/-

Na RAPHAEL OKELLO-BUNDA

KAMPUNI ya Olam Tanzania imewakopesha wakulima wa pamba, mbegu kilo 169,657 zenye thamani ya Sh milioni 118.7 katika msimu wa kilimo uliomalizika wa mwaka 2016/2017.

Meneja wa Zabuni wa Kampuni hiyo Mkoa wa Mara, Mariamu Mwinyi alisema katika mkopo huo deni lililolipwa hadi sasa lilikuwa  Sh milioni 81.3 na   bado  Sh milioni 37.4.

Alisema wakulima hao walikopeshwa kwa  utaratibu wa mpango wa kilimo cha mkataba cha pamba.

Mwinyi alisema kushindwa kulipa deni hilo kwa wakulima kutakwamisha kampuni hiyo kusambaza mbegu nyingine katika msimu ujao wa kilimo.

Mkaguzi wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) Wilaya ya Bunda, Liberatus Soka aliwashauri maofisa ugani, wenyeviti wa vijiji, watendaji na madiwani kuwahamasisha wakulima kutumia mbegu mpya za pamba za UKM 08 isiyo na manyoya ambayo ni bora.

Alisema mbegu hiyo mpya ni bora hivyo inapunguza gharama kwa wakulima kwa sababu  mkulima anaweza kupanda kilo sita kwa ekari moja tofauti na mbegu ya zamani   ya UK 91 yenye manyoya ambayo kwa ekari moja wanapanda kati ya kilo 15 mpaka 20.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili,  aliwapongeza wakulima  wa pamba   kwa kuuza pamba safi msimu uliopita.

Aliwataka wale wanaodaiwa kulipa deni hilo kabla ya mwisho wa mwezi huu  kampuni hiyo iweze kuandaa mbegu kwa ajili ya msimu ujao.

Hata hivyo  aliziagiza bodi za Shule za Sekondari na Kamati za Shule za Msingi kuanzisha mashamba darasa ya kilimo cha pamba kama hatua ya kukuza kilimo hicho.

Alisisitiza   hatua hiyo ianze kwa katika msimu huu wa kilimo.

Alisema agizo la Serikali ni kufufua upya kwa uzalishaji wa   pamba katika mikoa 10 hivyo ni lazima shule hizo kuwa na mashamba darasa kwa kuwa itasaidia pia kuwaingizia kipato.

Wadau  wa kilimo hicho wilayani Bunda walieleza changamoto  katika kilimo hicho wakitaja kuwa ni pembejeo kutofikishwa kwa wakati, ukame na baadhi  ya wakulima kutolipa madeni yao kwa wakati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles