27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

KAMANDA WA WAASI ASOMEWA MASHTAKA 70 ICC

Dominic Ongwen
Dominic Ongwen

THE HAGUE, UHOLANZI

MMOJA wa makamanda wa ngazi ya juu katika jeshi la waasi wa Uganda la Lord Resistance Army (LRA), Dominic Ongwen, jana amefikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), akikabiliwa na mashtaka 70 ya uhalifu wa kivita.

Ongwen anakabiliwa na mashitaka kadhaa ya mauaji, ubakaji na kuwatumia wanajeshi watoto wakati wa uasi wa kundi hilo, kesi ambayo inafuatiliwa kwa karibu na wahanga wa uasi wa kundi hilo.

Kamanda huyo ambaye sasa ana umri wa miaka 40, anakuwa askari wa kwanza wa zamani mtoto kushtakiwa katika mahakama hiyo kwa makosa hayo ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu ambayo yalifanywa na kundi hilo linaloongozwa na Joseph Kony.

“Uongozi wa LRA unajulikana duniani kote kwa ukatili wake dhidi ya Waafrika, lakini haijawahi kutokea kamanda yeyote wa LRA kushtakiwa,” alisema Elise Keppler kutoka Shirika la Haki za Binadamu na kuongeza kuwa kesi hiyo ni hatua moja muhimu.

Umoja wa Mataifa (UN) ulisema kundi hilo liliwaua watu zaidi ya 100,000 na kuwateka watoto 60,000 tangu lilipoanzisha uasi wenye umwagaji damu dhidi ya Serikali ya Uganda.

Zaidi ya waathirika 4,000 wanashiriki katika kesi ya Ongwen na maelfu wengine wanatarajiwa kufuatilia kesi hiyo kutokea kaskazini mwa Uganda kupitia televisheni.

Waathirika wanauelezea ukatili wa kundi hilo hasa kwa kuwateka nyara vijana wadogo na kuwalazimisha kuwaua na kuwapiga marafiki na ndugu zao wa familia hadi kufariki au kunywa damu yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles