26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

‘Kama maambukizi ya COVID-19 ndani ya jamii yamedhibitiwa, fungueni shule ‘– Guterres

New York, Marekani.


KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa tamko lake la kisera lenye lengo la kuhakikisha kuwa janga hilo halizidishi pengo lililokuwa la walio na elimu na wasio na elimu.


Tamko hilo amelitoa kwa njia ya video jijini New York, Marekani leo Agosti 4, pamoja na kuweka bayana changamoto za elimu zilizokuwepo kabla ya COVID-19 na baada ya COVID-19, ambapo ameeleza kuwa hata hatua zilizochukuliwa za kutoa elimu kwa njia ya televisheni na radio wakati huu ambapo shule zimefungwa bado zimeonesha pengo la wenye fursa na wasio na fursa.
“Katikati ya mwezi Jula

i, shule zilikuwa zimefungwa katika nchi zaidi ya 160 na kuathiri zaidi ya wanafunzi bilioni 1. Takribani watoto milioni 40 duniani kote wamekosa elimu yao muhimu ya awali. Na wazazi, hususan wanawake wamelazimika kubeba mzigo mzito wa malezi nyumbani.


“icha ya masomo kupelekwa kwa njia ya redio, televisheni na mtandaoni, na juhudi kubwa za walimu na wazazi, wanafunzi wengi bado hawajafikiwa. Wanafunzi wenye ulemavu, wale walio katika jamii ndogo au za pembezoni, wakimbizi wa ndani, wakimbizi na wale walio maeneo ya ndani wako hatarini kuachwa nyuma,” amesema Katibu Mkuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles