28.2 C
Dar es Salaam
Monday, July 4, 2022

Waziri wa kilimo aongeza siku mbili maonesho ya Nanenane

Derick Milton, Simiyu.

Kulingana na kuchelewa kuanza kwa maonesho ya sikukuu ya wakulima (Nanenane) Mwaka 2020 katika baadhi ya kanda serikali imetangaza kuongeza siku mbili za maonesho hayo ambapo yatahitimishwa Augosti 10,mwaka huu badala ya Agosti 8.

Uhaumuzi huo umetangazwa leo na Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga wakati alipotembelea Banda la Chama wajasaliamali wanawake Tanzania (TABWA) kwenye viwanja vya Maonesho ya wakulima (Nanenane) ambayo kitaifa yanafanyika Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Hasunga amesema kuwa kulingana na mahitaji ya sherehe za wakulima kujifunza mbinu bora za kilimo wananchi ambao hawakupata fursa awali watatumia nafasi hiyo kujionea mbinu bora za kilimo, mifugo na uvuvi na teknologia za kisasa.

Amesema kuwa kwenye kanda za Nanenane ambazo maonesho hayo yanafanyika, baadhi yake yalichelewa kuanza, hali ambayo Wizara yake imepata maombi mengi kutoka kwa wadau wakitaka kuongezwa siku.

“ Kwa mamlaka niliyonayo na maombi mengi ambayo nimepata kutoka kwa wadau, lakini pia baadhi ya kanda kuchelewa kuanza maonesho haya natanga rasmi leo kuongeza siku mbili za maonesho,” alisema Hasunga.

Amewataka wananchi wote nchini, wakiwemo wafugaji, wavuvi na wakulima kutumia fursa hiyo kwenda kujifunza zaidi, teknologia mpya za kilimo, uvuvi na ufugaji.

Amesema malengo makubwa ya sherehe hizo ni pamoja na kuwaunganisha wakulima, wafugaji, wavuvi na wanaushirika kusherehekea kwa pamoja ikiwa ni pamoja na kuonesha teknolojia ya zana bora za kilimo, Mifugo na Uvuvi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
195,637FollowersFollow
545,000SubscribersSubscribe

Latest Articles