25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

KALONZO MUSYOKA ARUDI NYUMBANI


NAIROBI, KENYA

KINARA mwenza wa muungano wa upinzani wa National Super Alliance (NASA), Kalonzo Musyoka amerudi nchini hapa kutoka Ujerumani alikokuwa akimuuguza mkewe.

Musyoka, ambaye alikuwa nje ya nchi tangu Oktoba 11 mwaka huu, aliwasili nyumbani akiwa na mkewe Pauline, ambaye afya yake imeripotiwa kuimarika.

Mkewe amekuwa akiugua tangu mwaka 2015 na Musyoka alilazimika kukatisha kampeni za Nasa za marudio ya uchaguzi wa urais wa Oktoba 26 ili aweze kuwa karibu na mkewe nchini Ujerumani.

Aliondoka siku moja tu baada ya upinzani ukiongozwa na mgombea urais wa Nasa, Raila Odinga kujitoa katika uchaguzi huo wa marudio kwa kile ulichodai kutotekelezwa kwa masharti ya kuruhusu uchaguzi huru na wa haki.

Makamu huyo wa rais leo anatarajia kutembelea nyumba ya Mbunge wa zamani wa Kitui magharibi Francis Nyenze, ambaye alizikwa wiki iliyopita.

Kuwasili kwa mgombea huyo mwenza wa Odinga kunakuja wakati NASA ikitishia kumuapisha urais Odinga na Musyoka kwa kile ulichodai ulishinda uchaguzi wa kwanza wa urais wa Agosti 8.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles