25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Kalemani awapongeza wafanyakazi Wizara ya Nishati na Taasisi zake

Na Mwandishi Weti, Dodoma

Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani amewapongeza wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa kufanya kazi kwa ufanisi ambao umechagiza nchi kuingia katika uchumi wa kati kutokana na uwepo wa nishati inayotabirika.

Dk.Kalemani ametoa pongezi hizo jijini Dodoma, Mei 5, 2021 wakati akifungua Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Nishati ambapo Mkutano huo uliongozwa na Mwenyekiti, Kheri Mahimbali ambaye ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara, Mhandisi Leonard Masanja.

“Wizara ya Nishati ni injini katika uchumi wa Taifa letu, huwezi kuzungumzia maendeleo bila kugusa masuala ya nishati, na nishati si umeme tu, bali kuna gesi, mafuta na nyinginezo, ujenzi wa uchumi wa viwanda vikubwa  na vidogo unategemea nishati kama vile ya umeme ambayo inachochea kwa haraka katika kujenga viwanda ambavyo vinasisitizwa katika uchumi huu wa kati,” amesema Dk.Kalemani.

Mwenyekiti wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Kheri Mahimbali akieleza umuhimu wa Kikao cha Baraza la Wafanayakazi wa Wizara hiyo kilichofanyika Mei 5, 2021 Jijini Dodoma.

Dk. Kalemani amewapongeza wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa kufanya kazi kwa ufanisi ambao umechagiza nchi kuingia katika uchumi wa kati kutokana na uwepo wa nishati inayotabirika.

Dkt.Kalemani ametoa pongezi hizo jijini Dodoma, Mei 5, 2021 wakati akifungua Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Nishati ambapo Mkutano huo uliongozwa na Mwenyekiti, Kheri Mahimbali ambaye ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara, Mhandisi Leonard Masanja.

“Wizara ya Nishati ni injini katika uchumi wa Taifa letu, huwezi kuzungumzia maendeleo bila kugusa masuala ya nishati, na nishati si umeme tu, bali kuna gesi, mafuta na nyinginezo, ujenzi wa uchumi wa viwanda vikubwa  na vidogo unategemea nishati kama vile ya umeme ambayo inachochea kwa haraka katika kujenga viwanda ambavyo vinasisitizwa katika uchumi huu wa kati,” amesema Dk.Kalemani.

Ameongeza kuwa, utendaji mzuri wa wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake umepelekea wananchi wengi kutumia umeme ambapo kwa sasa zaidi ya asilimia 80 ya watanzania wanatumia nishati hiyo, na hii inatokana na juhudi zinazofanywa na wafanyakazi hao.

Mbali ya pongezi hizo, Waziri wa Nishati amewataka wafanyakazi kufanya kazi kwa kasi, ubunifu na usahihi wenye weledi ili kuendelea kupata mafanikio na kujenga uchumi imara.

Watumishi wa Wizara ya Nishati wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nishati wakati wa hafla ya ufunguzi wa kikao cha Baraza la Wafanayakazi wa Wizara hiyo kilichofanyika Mei 5, 2021 Jijini Dodoma.

Aidha, amewaasa kuendelea kudumisha ushirikino kati ya Mfanyakazi na Muajiri  na kufanya kazi kwa  kuzingatia sheria, taratibu na kanuni ili kuongeza ufanisi.

Vilevile, amewasisitiza viongozi wa Wizara kuzingatia maslahi ya wafanyakazi ikiwemo kupandisha vyeo, madaraja na kulipa mafao ili kuwapa morali wafanyakazi ya kuchapa kazi zaidi.

Kwa upande wa wafanyakazi, alitoa angalizo la kutokufanya kazi kwa mazoea na badala yake kila mfanyakazi anapaswa kufanya kazi kwa bidii, ubunifu, kujituma, kasi na kuzingatia viwango.

Kuhusu masuala ya kipaumbele ya kimkakati yaliyopangwa na Wizara, ikiwemo utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere (MW 2115), ameagiza kuwa, yatekelezwe kwa wakati na Baraza la Wafanyakazi lihakikishe kuwa masuala hayo yanatekelezeka.

Aidha ameagiza kuwa, Baraza hilo lijadili na kutoa maoni kuhusu ufanikishaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ya usambazaji umeme katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo ya vijiji,  miradi ya gesi ukiwemo wa Kuchakata na Usindikaji Gesi asilia (LNG),  mradi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki na ujenzi wa miundombinu ya umeme katika Reli ya Kisasa (SGR).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles