32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Kafulila atoa wiki moja kwa Tanroads Simiyu

Na Derick Milton, Simiyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila, ametoa muda wa wiki moja kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) mkoani humo, Mhandisi Albert Kent, kufanya mchanganuo wa ushuru na mrabaha ambao unatakiwa kulipwa na Mkandarasi (CHICCO) kama tozo za kokoto, mawe na mchanga.

Hali ya Barabara ya Mwigumbi-Maswa mkoani Simiyu ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami na mkandarasi CHICCO ambapo imeanza kuharibika kabla ya ujenzi wake kukamilika lakini pia kabla ya kufunguliwa.

Mkandarasi huyo ambaye anatengeneza Barabara ya Mwigumbi – Maswa yenye urefu wa kilometa 50 kwa kiwango cha lami, anadaiwa kugoma kulipa tozo hizo kwa Halmashauri ambazo amekuwa akichukua malighafi hizo pamoja na Ofisi ya Madini kama sheria inavyotaka.

Kafulila ametoa maagizo hayo leo, Juni 1, 2021 wakati akikagua barabara hiyo kutokana na kuanza kuharibika kabla ya kufunguliwa.Kwani licha ya kukamilika kwa kiwango kikubwa, ambapo eneo kubwa limeanza kuwa na mashimo huku sababu kubwa ikielezwa kuwa kujengwa chini ya kiwango.

Amesema toka mwaka 2015 Mkandarasi huyo aanze kujenga barabara hiyo, amegoma kulipa ushuru kwa halmashauri ya Maswa, lakini pia mrabaha wa Ofisi ya Madini zaidi ya Sh milioni 600 huku Taroads wakilalamikiwa kushindwa kutoa ushirikiano ili tozo hio zilipwe.

Kabla ya kutoa maagizo hayo, Kafulila alimtaka Mkurugenzi wahalmashauri ya Maswa, Dk. Fredrick Segamiko, kutoa maelezo ya tatizo hilo, ambapo Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa wamehangaika sana kulipwa ushuru huo bila mafanikio.

Segamiko amemweleza Mkuu huyo wa mkoa kuwa, Ofisi yake imekuwa ikiomba ushirikiano kutoka Tanroads mkoa, lakini hawapati licha ya kwenda mara kwa mara na kueleza tatizo la mkandarasi huyo kushindwa kulipa ushuru kwa muda mrefu.

“Hadi jumatatu wiki ijayo nipate mchanganuo huo wa malipo hayo na mkandarasi analipa lini, Tanroads ndiyo wenye jukumu hili hampaswi kulikwepa kwa sababu nyie ndiyo mmewaleta hawa wakandarasi na wanatakiwa kufuata sheria,” amesema Kafulila.

Katika hatu nyingine Mkuu huyo wa ametoa onyo la mwisho kwa Tanroads juu ya wakandarasi wake kutokulipa tozo hizo za kisheria, ambapo ametaka kila mkandarasi ambaye atapewa kazi anatakiwa kuhakikisha analipa ushuru na mrabaha huo ndani ya muda.

” Tanroads hii iwe mara ya mwisho, leseni mnatoa ninyi alafu wanagoma kulipa kulipa ushuru na mrabaha, na mkiombwa kutoa ushirikiano mnagoma, tafsiri yake ni kuwa Tanroads mnawasaidia wakandarasi kukwepa kodi,” amesema Kafulila.

Aidha, Kafulila ametaka kusimamia kwa miradi ya serikali ili isijengwe chini ya kiwango Kama ambavyo imetokea kwenye Barabara hiyo huku akitoa onyo kutojirudia kwa uzembe huo kwenye miradi mingine.

Akizungumzia ubovu wa barabara hiyo, Mhandisi Kent amesema kuwa, Mkandarasi ameelekwezwa kurudia matengenezo katika maeneo yote ambayo yameharibika kwa kutumia gharama zake mwenyewe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles